Hitmaker wa Ngomani, Timbulo amedai hana bifu na Vanessa Mdee
aliyemchomolea kufanya naye collabo sambamba na Malaika aliyemchomolea
kufanya naye video ya Ngomani iliyomgharimu muda wa kuirudia ngoma hiyo
na Neylee na kisha kuifanyia video.
“Kitu kizuri niligundua tatizo liko wapi na kuli-solve. Collabo yangu
mimi ilikuwa inamsaidia Malaika kuonekana kwenye video yangu ilikuwa ni
msaada mkubwa sana kwake pia kwa sababu watu wangemuona na ilikuwa ni
nafasi yake nyingine kuongeza step nyingine ya mashabiki, lakini pia
kufanya kazi na Vanessa ilikuwa inamsaidia pia,” amesikika Timbulo
katika kipengele cha Pigia Mstari kupitia kipindi cha The Splash cha
Redio Ebony FM ya Iringa.
Timbulo ameongeza kuwa “Yaani kila kazi ambayo msanii unaifanya baina
ya mimi inakuongea step moja ya kwenda mbele so ukiwa na hiyo imani
daima huwezi kuzingua kwenye kazi ya msanii ambae unaona kabisa msanii
anayefahamika na ana nafasi kubwa kwenye gemu.”
Kwa upande Mwingine Timbulo amewataka mashabiki wake na muziki wa
Bongo Flava kwa Ujumla kukaa vema kwa ujio wake mpya unaotoka mwezi huu
wa Novemba.
“Tutakuwa tunasomana katika media zote naamini ni project kubwa sana
ambayo pengine sijawahi kuifanya kwa sababu ya aina ya muziki ambao
nimeufanya, lakini pia ni project yangu ya kwanza kufanya nje ya
Tanzania nazungumzia video, so ni kitu kikubwa kila kitu kimefanyika kwa
ufanisi wa hali ya juu kwenye ubora wake ambao mimi sijawahi kufanya
nathubutu kusema hivyo” amesema Timbulo .
0 maoni: