Mtayarishaji wa video za muziki nchini, Hanscana amewataka wasanii wa
muziki nchini kuanza kuwaamini madirector wachanga ili kuwapa nafasi ya
kuonyesha uwezo wao.
Mwongozaji huyo amesema wasanii wengi wamekuwa wakiangalia uzoefu na
majina kitu ambacho kinawanyima fursa madirector wachanga wenye vipaji.
“Ufike wakati wasanii muanze kuamini talent, uwezo na sio jina kama
ilivyozoeleka na mimi naamini sana uwezo wa madirector wachanga ambao
wanaanza,” aliandika Hanscana Instagram.
Aliongeza, “Hivyo basi ifike time nawao pia waaminiwe na wapewe
videos kubwa ili kuendelea kusogeza sanaa yetu mbele na iwe ya
kiushindani zaidi kama zilivyo South Africa na Nigeria,”
Hanscana ambaye amefanya video nyingi za masta wa muziki ndani ya
mwaka 2016, amemtabiria makubwa director mchanga aitwae hopefx.
Related Posts:
Abdu Kiba awaonya Diamond na Alikiba ‘kuna madogo wamejipanga kuchukua nafasi zenu’ (Video) Abdu Kiba anaamini kuwa, pamoja na kwamba kaka yake Alikiba na hasimu… Read More
Mimi nafanya kazi kama kichaa – Vanessa Mdee Msanii wa muziki Vanessa Mdee amefunguka kwa kudai kuwa yeye ni mmoja… Read More
Video: Diamond aporomosha matusi mazito kwenye Instagram Live Instagram Live inawapa uchizi mastaa na kadri siku zinavyokwenda, … Read More
Picha: Nicki Minaj na Drake wapiga picha ya pamoja baada ya kupita miaka miwili Ni muda mrefu Nicki Minaj na Drake hawajaonekana katika picha ya pamo… Read More