Home
NEWS
SUPER SOUL SUNDAY:Hii Ndo List ya watu waliowahi Kufanya Mambo makubwa Duniani
SUPER SOUL SUNDAY:Hii Ndo List ya watu waliowahi Kufanya Mambo makubwa Duniani
Kama ilivyokawaida kazi yangu kila Jumapili ni kukuletea nukuu saba
kutoka kwa watu ambao wamefanya mambo makubwa au ya kipekee katika
ulimwengu huu. Leo nimekuletea walichosema watu wenye nguvu ushawishi
duniani kuhusu mapenzi/upendo.
- Maisha bila upendo ni sawa na samaki bila bahari, ni kama anga bila nyota, na hata mwili bila roho – Delno L. A. Tromp.
- Hazina ya upendo unayoipata zaidi sasa itaishi kwa muda mrefu baada
ya dhahabu yako na afya njema pindi zitakapokuwa zimeharibika – Og Mandino.
- Mapenzi ni maisha… kama utakosa mapenzi, basi umekosa maisha –Leo Buscaglia.
- Ikiwa una upendo huhitaji kuwa na kitu kingine chochote, kama huna haijalishi nini kingine unacho – Sir James M. Barrie.
- . Si kwa kiwango gani tunafanya, bali ni upendo wa kiasi gani
tunauweka katika kile tunachofanya. Haijalishi tunatoa kiasi gani, bali
tunatoa kwa upendo wa kiasi gani – Mother Teresa.
- Kadiri unavyojifunnza kupenda, ndivyo unajifunza namna ya kuishi – Unknown.
- Jipende wewe mwenyewe kabla ya kumpenda mwingine, kwani kumpenda mwingine kabla yako haiwezekani – Jacob Gelt Dekker.
0 maoni: