Dereva wa Mbunge ashambuliwa na watu wasiojulikana

Dereva wa Mbunge John Heche wa CHADEMA, amevamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na kukatwa mapanga Mjini Tarime majira ya saa 2 usiku na hali yake siyo nzuri.
 
Mbunge John Heche amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kutokana na taarifa alizopata kupitia Katibu wake, Mrimi Zablon ambaye amekiri Dereva huyo anayefahamika kwa jina la Suez Daniel Maradufu ni kweli amepata shambulio hilo na sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu.
Dereva huyo amevamiwa na watu wasiojulikana na kumkata kwa mapanga kichwani na hali yake sio nzuri lakini anaendelea na matibabu kwenye Hospital ya Bomani Tarime.

0 maoni: