Nuh Mziwanda aaamua kuweka nguvu kwenye kipaji chake cha utayarishaji muziki

Nuh Mziwanda amesema kwa sasa amefikiria kujikita pia kwenye utayarishaji wa muziki, kitu ambacho amekuwa akikifanya kwa muda sasa.

Kupitia kipindi cha Zero Planet ya Ice Fm Njombe, mzazi huyo wa Binti Anyagile ametujuza juu ya lebo yake.
“Nimeamua kufanya kazi zangu mwenyewe kwasababu Jike shupa nilitengeneza mwenyewe lakini nikahamishia kwa Mr T, nikaona kwanini nawapa credit maproducer wengine wakati mimi nina kitu kikubwa kuliko wao? Ndio maana nikaamua kufungua record label yangu studio yangu na sasa hivi nasimama Nuh kama producer na Nuh kama
Kuhusu kuwa na mipango ya kusimamia wasanii, Nuh amesema, “Kuna wasanii nawamiliki kwenye label yangu wapo wawili kuna Chichi Chadala na Kompyuta, huyo kompyuta ndio ameandika wimbo wa Anamelemeta.” Boss huyo wa Last Born Records (LB) amewataka mashabiki kukaa mkao wa kula na baada ya mwezi mmoja wataachia kazi za wasanii wake pia.