Galaxy amfagilia Hanscana, adai video ya ‘Top In my Heart’ iliahirishwa mara 3

Bila umahiri wa Hanscana video ya ‘Top In my Heart’ wa Galaxy usingekuwa kama ilivyokuwa. Muimbaji huyo amefunguka kuwa waliahirisha mara tatu kushoot video ya wimbo huo kutokana na baadhi ya vitu kutokuwa sawa.

Akiongea na Bongo5, Galaxy amesema, “Video ya ‘Top In My Heart’ ndio video iliyonichanganya sana kuliko video zangu zote.
“Nilishoot kwa mara ya kwanza Afrika kusini lakini ilikuwa haijafikia kiwango tulichokuwa tunahitaji. Tulipokuja kushoot Bongo tuliahirisha mara tatu mfululizo, tulikuwa tunaenda location na kurudi kila siku. Napenda kusema ni juhudi binafsi za Hanscana lakini angekuwa director mwingine asiyependa kazi yake angeshoot ilimradi amalize tu. Lakini alitaka kitu kizuri kama tulivyokuwa tunataka,” ameongeza.
Wiki chache zilizopita muimbaji huyo aliahidi kuachia remix ya wimbo huo ambao amemshirikisha msanii kutoka Nigeria.