Video ya Eric Omondi yamtoa povu Barakah The Prince


Baada ya Eric Omondi kuachia video ya parody ya wimbo wa ‘Kuliko Jana’ wa Sauti Sol, msanii wa Bongo Fleva Barakah The Prince amemjia juu mchekeshaji huyo.
15101563_1134229833359198_5851538889465921536_n
Hitmaker huyo wa Nisamehe ameonyeshwa kuchukizwa na baadhi ya vipande vya kwenye video hiyo na kuamua kuweka wazi kupitia mtandao wa Instagram.
Kupitia mtandao huo, Barakah ameandika:
Ukiona unakosa cha kuchekesha watu bora utafute kazi nyingine ya kufanya kuliko alichofanya huyu sijui ndio anaitwa nan…kawakosea sana watu wote wenye imani ya kikristo…tafuta kazi nyingine… maana vichekesho nahisi umefikia mwisho…huyu jamaaa kafanya asubuhi yangu kuwa mbaya sana..shukuru wakristo ni wapole..ukifanya kitu ichi kwa Muslim..ungefanywa mfano..

0 maoni: