Tovuti hiyo imedai kuwa kuna dalili za wanandoa hao kusuluhisha matatizo yao na kuendelea kuwa pamoja ni kubwa.
Ripoti mpya imedai kuwa wawili hao wamekuwa kwenye maelewano mazuri tangu Tiny adai talaka yake, Dec. 7 na wamekuwa pamoja kwa ukaribu zaidi, kwa mujibu wa vyanzo. Wamedaiwa pia kusherehekea sikukuu ya Christmas pamoja na familia yao.
Wamekuwa pamoja kwa miaka 20 lakini walifunga ndoa rasmi mwaka 2010 na hadi sasa wana watoto watatu pamoja, King, Major, na Heiress Harris huku T.I. akiwa na watoto wengine wa nje ya ndoa, Messiah, Domani, na Deyjah Harris na Tiny ana binti aliyemzaa kwenye uhusiano uliopita, Zonnique Pullins