Christian Bella aeleza vitu vinavyokuja baada ya kukamilika kwa studio yake ‘Kingdom Music’ (Video)

Muimbaji huyo Alhamisi hii aliialika Bongo5 kuitembelea studio hiyo mpya iliyopo Sinza Palestina jijini Dar es salaam ili kujionea uwekezaji aliofanyika.
Bella ameiambia Bongo5 kuwa studio hiyo itamfanya afanye kazi zake kwa utulivu zaidi tofauti na awali.
“Lengo la kwanza la kuanzisha hii studio nilikuwa nataka nipate muda wakutosha wakufanya kazi zangu, kwamba hata saa sita usiku nikipata idea ninafungua studio nafanya kazi,” alisema Bella “Sio mpaka uanze kumtafuta producer ambaye anakupa promise ya wiki ijayo mpaka filling zinaondoka. Lakini sasa hivi nikipata filling hata saa nane usiku naingia studio nafanya kazi kwa sababu ipo kwajili yangu,”
Aliongeza, “Cha pili ni kusaidia vipaji pamoja na biashara, kwa wanaotaka kuja kurekodi mimi nawakaribisha tena nitakuwa natoa mchango hata wamawazo hata nikitakiwa kufanya nao kolabo nitaangalia mtu ambaye anafaa nitafanya naye,”
Pia muimbaji huyo amesema kukamilika kwa studio kunamfanya aanze mara moja mchakato wa kuandaa albamu yake mpya ambayo itakuwa na kolabo za mastaa wa nje.

0 maoni: