Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo “Kajiandae” akiwa na
Alikiba amesema kuwa presha za mashabiki ndio zinasababisha nyimbo za
wasanii kupotea mapema na kuwafanya waachie nyimbo nyingi kwa muda mfupi
tofauti na zamani ilivyokuwa.
“Unajua ushindani wa sasa hivi na wazamani umebadilika. Zamani
ulikuwa unaweza kutoa wimbo kwa muda mrefu ukakaa lakini sasa hivi
imekuwa watu wiki nyimbo, wiki nyimbo japo mimi siupendi sana huo
utaratibu kiukweli,” Ommy amekiambia kipindi cha The Playlist cha Tmies
FM.
“Naona si utaratibu mzuri kwa sababu hauzipi nyimbo zako nafasi,
unainvest matokeo yake nyimbo zinakufa mapema. Tusifanye nyimbo kwa
presha yaani sometimes mashabiki pia wanatupa presha sana, inabidi
waelewe kwamba kuna kuinvest hela nyingi, shabiki anachotaka yeye raha
umridhishe lakini pia shabiki anatakiwa aelewe video zinacost hela
nyingi,” ameongeza.
Dimpoz ameongeza kuwa walau msanii anatakiwa atoe nyimbo kila baada
ya miezi mitatu ili kuzipa nafasi nyimbo zake nyingine zilizopita.
0 maoni: