Miaka ya hivi karibuni mastaa kibao wametambua umuhimu wa kufanya mazoezi kujiweka vizuri kiafya na stamina.
Producer mkongwe wa Bongo Records, P-Funk Majani ni miongoni mwa mastaa wanaonyanyua vyuma
Ommy Dimpoz naye ameingia kwenye orodha hiyo ya wahudhuriaji wazuri wa gym.
Na sasa gym zimepata members wapya. Ni AY na Barnaba. Kama ulibahatika kukutana na AY hivi karibuni utagundua kuwa alikuwa amegain sana kiasi cha wengi kumshauri aanze kufanya mazoezi na sasa ameuzingatia na kuanzisha mkakati wa kuupunguza mwili wake.
Akipost picha akiwa kwenye gym, AY ameandika: Monday- Saturday #HitTheGymBeforeMasinema 90kgs –> 85kgs now heading to 75kgs Really Quick.. Blessings kwa @arnoldluciano & @ibra_carter.”
AY akiwa gym
0 maoni: