Ommy Dimpoz amesema alichangia kuandika hit single ya Diamond, Nasema Nawe – kipindi bado ni marafiki.
“Mimi nataka kusema kitu kimoja, sijawahi kusema sehemu yoyote hapa,
mfano kwenye nyimbo ya mduara ya D Nasema Nawe, mimi nimechangia kwa
asilimia kubwwa uandishi wa ile nyimbo. Sio kwamba D hajui kuandika,
anaandika vizuri na nawaheshimu ni moja ya waandishi bora kabisa,” Ommy
alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, Alhamis hii.
Ametolea mfano mstari aliochangia ni wa verse ya pili usemao
‘zingifuli zingifuli usozinga mahala ukakaa.’ Muimbaji huyo amesema hata
kwenye verse ya kwanza kuna maneno ameyaandika lakini hakuwahi kutaka
apewe credit.
“Sikufanya vile kwasababu nilipwe au nipewe credit. Lakini nataka tu
niseme kuwa mashabiki kuna vitu vingine vingi hawajui,” alisisitiza.
0 maoni: