WAANDAAJI
wa tuzo za muziki na filamu za EATV, EATV LTD jana walitangaza tano
bora ya wanaowania tuzo za muziki katika vipengele vitatu.
Waliotangazwa
jana kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es
Salaam na kurushwa moja kwa moja na kituo cha EATV na East Africa Radio
wanaungana na wasanii wengine kwenye vipengele tofauti waliotangazwa
mwanzoni mwa wiki hii.
Akizungumza
kwenye mkutano huo, Mkuu wa masoko wa EATV Ltd, Roy Mbowe, alisema
baada ya jopo la wataalam 30 wa muziki kukaa pamoja na kuchuja majina ya
wasanii waliojipendekeza kushiriki tuzo hizo wamepata majina ya
wanamuziki na wasanii wa filamu watakaowania tuzo hizo kubwa katika
ukanda huu wa Afrika Mashariki.
“Kura
kwa wasanii hawa zitaanza kupigwa kuanzia kesho ambapo kwa wale
watakatumia simu watatuma kura kwa namba 15777,” alisema Mbowe.
Aliwataja wasanii waliongia kwenye mchakato wa kupigiwa kura kwenye kipengele cha
Wimbo bora wa mwaka:
Joh Makini (Don’t Bother),
Lady Jaydee (ndi ndi ndi),
Navy Kenzo (Kamatia chini),
Ali Kiba (Aje)
Ben Pol (Moyo mashine).
Mwanamuziki bora wa kiume:
G-nako,
Sheath,
Ben Pol,
Mwana FA
Ali Kiba.
Mwanamuziki bora wa kike:
Lilian Mbabazi (Uganda),
Ruby,
Liana,
Vanessa Mdee
Lady Jay Dee.
Mwanamuziki bora Chipuki:
Man Fongo,
Feza Kessy ‘Feza’,
Rucky Baby,
Mayunga
Bright.
Muigizaji bora wa kiume:
Said Ally,
Meya Hamns,
Daudi Tairo ‘Duma’,
Salim Issa ‘Gabo’,
Doto Matotola.
Muigizaji bora wa kike:
Chuchu Hans,
Khadija Ally,
Kajala Masanja,
Rachel Bitulo
Khadija Ally.
Filamu bora ya mwaka:
Hii ni laana (Kajala Masanja),
Nimekosea wapi (Rachel Kitulo),
Safari ya Gwaru (Gabo),
Mfadhili Wangu (Daud Michael),
Facebook (Meya khamis).
Video ya Wimbo bora ya mwaka:
Ndi ndi ndi (Lady Jay Dee),
Don’t Bother (Joh Makini),
Aje (Ali Kiba),
Namjua (Shettah),
Njogereza (Navio).
Kundi bora la mwaka:
Wakali wao,
Sauti Sol (Kenya),
Team Mistari (Kenya),
Mashauzi Classic
Navy Kenzo.
Hafla ya utoaji wa tuzo hizo itafanyika Desemba 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
0 maoni: