Aunt Ezekiel akiwa na familia yake yake.
Party hiyo iliandaliwa na watangazaji wa kipindi cha SHILAWADU zamani ‘The Weekend Chart Show’ cha Clouds TV, Qwhisar pamoja na Soudy Brown katika hatua ya kuwashukuru mashabiki wa kipindi hicho.
Akiongea na waandishi mmoja kati ya watangazaji hao, Qwhisar alisema wamefanya party hiyo ili kuzungumza na mashabiki wa kipindi chao pamoja na kuwaambia maboresho mapya ambayo yatafanyika ndani mwaka 2017.
“Tunawashukuru sana mashabiki wa kipindi chetu kwa mapenzi makubwa tulioyaona ndani ya mwaka 2016, kipindi kinakuwa kikubwa kila siku na hali hiyo imetufanya tujipange zaidi kufanya mambo makubwa mwaka 2017. Kwa hiyo kuna mengi mazuri ndani ya SHILAWADU yanakuja,” alisema Qwhisar.
Kwa upande wa Soudy Brown ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha U Heard cha XXL ya Clouds FM, amedai ndani ya mwaka 2017 kuna maboresho makubwa yanafanyika ndani ya kupindi hicho. Angalia picha.
Msanii wa muziki Killy akitoa burudani katika party hiyo
Watoto wakiwa katika furaha