Nape kuhusu kelele za Diamond kukabidhiwa bendera: Watanzania tunahangaika na vitu visivyo na msingi



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema ameshangazwa na kelele zilizozalishwa kutokana na wiki hii kumkabidhi Diamond bendera ya taifa akijiandaa kwenye kutumbuiza kwenye ufunguzi wa michuano ya kombe la mataifa ya Africa nchini Gabon.

“Mambo mengine ni ya ajabu sana, sana, sana, watanzania wakati mwingine tunahangaika na vitu ambavyo wala havina msingi,” Nape alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.
“Tukijibu yote, tunaentertain tabia ya watu kuhangaika na vitu vya kijinga. Mwaka wakati kuna kombe la dunia South Africa, alialikwa Shakira kwenda kutumbuiza pale South Africa, nendeni mkagoogle, alikwenda na bendera za nchi yake cha ajabu ni nini?”
“Ndio maana ninasema tunahangaika na vitu vidogo sana badala ya kuhangaika na mambo makubwa. Siwezi kufanya jambo ambalo haliko sahihi kwa taarifa yako niko makini sana kuliko wanavyodhani,” alisisitiza.