Kwa sasa wasanii wengi wa muziki Bongo wamekuwa na msukumo mkubwa wa kuachia albamu huku Navy Kenzo wakiwa wamefungua njia hiyo baada ya kufungwa kwa miaka mingi. Joh Makini amefunguka pia kuhusu mipango yake wa kuachia albamu yake mwaka huu.
Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa mpaka sasa ana albamu mbili ambazo zipo tayari ila hajajua muda wa kuachia. “Ndio, mipango hiyo ipo, mimi binafsi nina albamu mbili. Nikiwa tayari nitasema,” amesema Joh.
Hitmaker huyo wa Perfect Combo ameongeza kuwa mashabiki watulie kuhusu kolabo zake alizofanya na Falz, Davido na YCEE (wote kutoka Nigeria) watazisikia kwa kuwa amezifanya nyimbo hizo kwa ajili yao.