Katika kitu ambacho teknolojia ya mawasiliano imesaidia kwenye muziki, ni uwezo wa mashabiki kuwa na access ya kutoa maoni yao kwa kazi za wasanii, punde zinapotoka.
Wakati mwingine mashabiki huwa si wachaguzi wazuri wa lugha wanayotumia kuwasilisha ujumbe wao na hivyo baadhi ya maoni hasi huwavunja sana moyo wasanii.
Kwa upande wa Ben Pol, amedai kuwa maoni ya haraka na papo kwa papo baada ya wimbo wake kutoka huwa hayazingatii na huyaepuka kuyasoma hasa yakiwa hasi.
“Nimeupload video ina dakika 5, mtu ameshaweka pale ‘ahh nyimbo mbovu, huwa simsikilizi kabisa kwasababu wale wale watu baadaye after two weeks, wanarudi wanasema ‘kaka ebana ehh, hii ngoma nimechelewa kweli kuielewa, kumbe bonge la ngoma. Ebana hii ngoma watu nimebishana nayo sasa hivi ndio nimeona kweli bonge la ngoma.’ Kwahiyo wale watu baadaye wanakujaga wanajizawazisha wenyewe, wakisikiliza mara mbili mara tatu wanajua kwamba walikurupuka,” Ben Pol ameiambia Bongo5.
Muimbaji huyo amedai kuwa huyazingatia zaidi maoni ya watu ambao huchukua muda kuusikiliza na wakauelewa vyema wimbo wake. Amedai kuwa mara nyingi nyimbo anazotoa yeye, huwa zimesikilizwa kwanza na watu zaidi ya 20 ambao hutoa maoni yao kumshauri wimbo wa kuutoa.
Kingine Ben Pol amesema wimbo mzuri haujifichi, na reaction yake huonekana bila hata kujihangaisha. “Comments mbaya na nzuri lazima zitakuwepo, lakini kama wimbo unafanya vizuri, utauona tu kwamba unafanya vizuri na haitakiwi kukudiscourage endapo haujafanya vizuri.”
Amesisitiza kuwa kila wimbo huwa na mapokeo yanayotofautiana.