Wabogojo alivyoisaidia Muziki ya Darassa kupaa kimataifa, soma maoni ya mashabiki nje ya TZ

Mwaka 2016 unamalizika ukiwa na historia ambayo haitosahaulika kwenye maisha ya muziki ya rapper Darassa. Rapper huyo amefanikiwa kutengeneza wimbo namba moja Tanzania kwa sasa huku pia umaarufu wa wimbo huo ukiendelea kusambaa kwa kasi ya ajabu katika nchi zingine. Tunavyozungumza sasa, wimbo huo ni moja ya nyimbo kubwa Kenya na kinachofurahisha zaidi, Wakenya wameupenda kwakuwa una ladha ya muziki wa Kapuka na baadhi ya mashairi yake yamewafanya wafikirie kuwa ana asili ya Kenya!! Lakini kuna mtu mmoja muhimu ambaye Darassa na Ben Pol wanapaswa kumshukuru kwa kusaidia kuupaisha wimbo huo nje ya mipaka ya Tanzania. Si mwingine ni mchekeshaji na mcheza sarakasi, Wabogojo. Wiki tatu zilizopita, mchekeshaji huyo alipost video akiwa amejifunga taulo la pinki na mswaki mdomoni akiucheza wimbo huo kwa mbwembwe nyingi. Ndani ya muda mfupi, video hiyo ilisambaa mtandaoni hasa Facebook na Instagram na watu wengi nje ya Tanzania wakaiona. Umaarufu wa video hiyo uliwafanya watu waende Youtube kuutazama wimbo mwenyewe na kujikuta wakipenda walichokiona na kukisikia. Wengi wameeleza kwenye video ya Darassa kuwa wameenda kuitazama baada ya kuiona video ya Wabogojo ambaye wamempa jina ‘The Guy With A Pink Towel.’ Hawa ni miongoni mwao:
Dellen Ward
The Somalian boy in the pink towel dancing brought me here
Sheba Okorey
Guy dancing in a pink towel brought me here…Big tuneee.
Sarah Ndumbu
Woooow niliona jamaa wa towel ya pink akidance hii song mpaka imebidi niitafute. I love It from kenya
Susan Machau
The skinny guy who was playing this song with a pink towel amefanya watu wengi kufollow hii ngoma.. It’s dope
Saba
The crazy dude wearing a pink towel on facebook brought me here
Lucas Wanjala
the dude with pink towel made this song famous,nice track
Ali Jalay
I SEE THAT GUY IN THE PINK TOWEL BROUGHT A LOT OF PEOPLE TOGETHER.

Help Me Get 50 Subs With No Videos

Am I the only one who’s here because of facebook with that skinny ass nigga that was dancing!!
Edna zaato
Man in pink towel video from instagram. Anyone ? lmao
mart_254 Molohills
The skinny dude wth pink towel brought me here his instagram handle is wabogojoford thank me later
Dialysis Technicians WorldWide
Guy with pink towel brought me here to hear the whole version.

Related Posts: