Video: M-Rap aelezea jinsi ngoma yake na Mayunga inavyopeta nje

Wimbo mpya wa rapper M-Rap aliomshirikisha Mayunga unaitwa Ts No Too Late, na huenda ukawa na maana kuwa hajachelewa kuonekana kimataifa baada ya kusota kwa muda sasa.
Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa licha ya wimbo huo kufanya vizuri nchini, umepokelewa kwa mikono miwili na channel kubwa za runinga Afrika. Ameushukuru uongozi wake, Mukii International kwa kumwezesha kuyafikia matawi ambayo alikuwa akiyasikia tu kufikiwa na wasanii wengine. “Sijawahi kupata coverage kubwa ya wimbo wangu katika nchi za Afrika kama huu hapa,” amesema. “Kwasababu sasa hivi unapigwa huko sehemu za nje na watu wanaappreciate. Hiyo yote imewezekana kwasababu wanahitaji quality, wanahitaji muziki mzuri ambao production yake ni nzuri,” ameongeza. M-Rap amesema video yake inachezwa sana Trace Naija na itaanza kuoneshwa kwenye channel zingine. Kwa upande wa Mukii International, rapper huyo amesema kwa sasa ina wasanii watatu, wengine wakiwa Miss Rizy huku hivi karibuni wakimuongeza Miss Universe, Jihan Dimack.