Akijibu swali la mmoja kati ya mashabiki ambao walijitokeza jana Mlimani City ambalo lilihoji label ya WCB imejipanga vipi kuendelea kusaini wasanii wapya, Sallam alidai wao kama WCB watakuwa wanadeal na label na sio msanii mmoja mmoja.
“Kwa sasa tunasaini na label,” alisema Sallam. “Kwa hiyo label ambayo utakuwa wewe itakuwa chini ya WCB na WCB kazi zako tutazipeleka mbali kabisa,”.
Aliongeza,”Tukiwachukua wasanii wote WCB peke yake, tutakuwa wachoyo na sisi hatutaki kuwa wachoyo. Kwa hiyo label nyingi zifunguke na WCB tutadeal na label hatuwezi kudeal na msanii mmoja mmoja kwa sababu nauhakika milioni 10 ya watanzania ni wasanii,”
Kwa sasa label ya WCB ina miliki wasanii wanne, Rich Mavoko, Rayvanny, Harmonize pamoja na Queen Daren.