Drake na J.Lo wasample wimbo wa Black Coffee wa SA

Wakati tetesi za uhusiano wa kimapenzi kati ya Drake na Jennifer Lopez zikizidi kushamiri, wawili hao wameonekana wakicheza na kusikiliza wimbo waliofanya pamoja. Wimbo huo umesample ngoma ya DJ wa Afrika Kusini, Black Coffee, Superman. Hafla hiyo iliyopewa jina la Winter Wonderland Prom na mwenyeji wake akiwa J.Lo huko Hollywood. Drake aliwahi kumsifia Black Coffee kwenye OVO Sound Radio July 2015.