Dj Funkmaster Flex aingia tena kwenye bifu na Drake, kisa ni J.Lo

Dj maarufu wa redio ya Hot 97, Funkmaster Flex ameendeleza bifu zake na mastaa wakubwa – na sasa amerudi tena kwa Drake.

Funk ameanzisha ugomvi huo Alhamisi hii kupitia mtandao wa Twitter baada ya kusambaa kwa picha mpya ya Drake na Jennifer Lopez ambayo imezidi kuongeza uvumi kuwa wawili hao ni wapenzi.
Hizi ni baadhi ya tweete za Dj huyo.

Hii ni mara ya pili kwa Funkmaster kuingia kwenye bifu na Drake na wiki mbili zilizopita aliingia kwenye vita ya maneno na Bow Wow baada ya kumwambia msanii huyo hajielewi na hafanyi vizuri kutokana na albamu zake hazinunuliwi na mashabiki.

Related Posts: